,

,

Join The Community

Premium WordPress Themes

Thursday, October 2, 2014

Taarifa Kwa Umma Kutoka Cham Cha ACT-TANZANIA Kuhusu Zitto Kabwe na Chama Cha ACT- Tanzania


 Zitto Kabwe
--
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY. 
--
Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.


Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".Act-Tanzania tunaeleza kuwa ni chama cha watanzania wote kisichokuwa na mmilki wake na tunaunganishwa na misingi kumi ya chama pamoja na Itikadi yetu ya Demokrasia jamii.

Act-Tanzania tunatambua uwezo na mchango wa kisiasa na ujenzi wa demokrasia ya vyama vyingi nchini uliotolewa na Mheshimiwa Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Na kwamba kwa sasa ana kesi na chama chake mahakamani na tunaamini atakapomaliza kesi hiyo mchango wake katika siasa za upinzani za Tanzania ni muhimu sana.

Act-Tanzania tunaamini kwamba Mheshimiwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa mahiri na makini hivyo tunamkaribisha kwa moyo mkunjufu katika chama mbadala Tanzania.

Na kuhusiana kwamba kuna mkakati wa kuipa nguvu Act-Tanzania ni taarifa za kutunga kwani mikakati yetu ya kuimarisha chama na uenezi wake ni mkubwa na mipango yetu inayotekelezwa kwa umakini na weledi mkubwa.

Na Act-Tanzania tumejipanga kufanya siasa zitakazoleta mabadiliko nchini na kasi yetu inatokana na juhudi na mshikamano wa viongozi wa ngazi zote.

Aidha tunatumia eneo kubwa la mipango yetu ya kukieneza chama kwa mfano kwa sasa tumemaliza ziara ya mikoa 12 na majimbo 68 hivi karibuni iliyokuwa na mafanikio makubwa sana.

Pamoja na mambo mengine tulitoa maelekezo ya maandalizi ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na serikali za mitaa tarehe 14/12/2014,tukitekeleza azimio la kikao cha Halmashauri kuu kilichofanyika Singida.

Hivyo hakuna mkakati wa kuibeba ACT-Tanzania,Bali ACT-Tanzania inabebwa na umakini na weledi katika mipango yake.

Kuhusu Bwana Samson Mwigamba na Profesa Kitilia Nkumbo kujiunga na Act-Tanzania hawa ni watanzania na baada ya kufukuzwa na chama chao cha zamani Act-Tanzania tuliona mchango wao bado unahitajika katika siasa hapa nchini na kwa kuwa hakukuwa na kizuizi kwa wao kujiunga na Act-Tanzania basi tuliwapokea na kwa sasa wanatumikia Act-Tanzania kwa moyo wa kizalendo kabisa.

Kuhusiana na hoja ya kwamba kuna mamluki wa upinzani hizo ni siasa nyepesi kwani unapofukuza wanasiasa mahiri ndani ya chama chochote na wanapokosa fursa ya kufanya siasa pale walipofukuzwa hakuna dhambi ya kushiriki siasa katika chama kipya cha siasa hapa nchini.

Mwisho tunawashukuru watanzania wote wanaoendelea kutuunga mkono nchini kote.

Pia tunapenda kutoa tamko kwamba kwa mujibu wa maazimio ya kikao cha Halmashauri kuu kilichokutana mjini Singida tarehe 25-26/7/2014 tunaendelea na maandalizi ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na serikali za mitaa na maandalizi yetu yanaendelea vyema kabisa.

Lakini pia tunaheshimu uhuru wa kutoa habari waliotumia gazeti la mwanahabari lakini tumesikitishwa sana na wao kama chombo huru kushindwa kutuhoji sisi kama chama baada ya kuwa na habari wanayoiita "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".

Imetolewa Leo tarehe 01/10/2014
Na Mohammed Massaga
Katibu mawasiliano na Uenezi wa ACT-TANZANIA Taifa
0718388888.

PICHA NA TAARIFA RASMI KUTOKA IKULU:RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA RASMI BARABARA YA MWENGE-TEGETA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

  Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa tayari tayari kumrekodi Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua  rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakifurahia baada ya kufungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es salaam Ndg Ramadhani Madabida
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine. PICHA NA IKULU
----
Jumatano, Oktoba Mosi, 2014, amezindua rasmi Barabara ya Kisasa ya Mwenge-Tegeta ambayo ni sehemu ya Barabara ya New Bagamoyo Road, mjini Dar Es Salaam.
 

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12.9 imegharimu kiasi cha Sh. bilioni 77.85, fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa la JICA. Serikali ya Tanzania imechangia asilimia 7.64 katika gharama za ujenzi wa Barabara hiyo.

Rais Kikwete amefanya uzinduzi huo katika eneo la Makutano ya Kambi ya Jeshi ya Lugalo na Barabara ya Kawe katika sherehe iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi. Alikuwa ni Rais Kikwete ambaye aliweke jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara hiyo Aprili 4, mwaka 2011.

Barabara hiyo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa Barabara itokayo Makutano ya Barabara ya Kawawa, Kinondoni hadi Tegeta. Ujenzi wa awamu ya pili wa kilomita 4.3 kati ya Mwenge na Makutano ya Barabara ya Kawawa, unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya mipango yote ya ujenzi huo kukamilika.

Barabara hiyo ya Mwenge-Tegeta inalenga kupunguza msongamano wa magari katika eneo la kaskazini mwa Dar Es Salaam na pia ni sehemu ya bararaba kuu inayounganisha Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani, kupitia Wilaya ya Bagamoyo, na kuunganisha mikoa hiyo na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa Barabara hiyo iliyojengwa na Kampuni ya Konoike kutoka pia Japan, Balozi wa Japan katika Tanzania, Mheshimiwa Masaki Okada amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulichelewa kukamilika mwaka jana, kama ilivyopangwa, kwa sababu ya wajenzi kukabiliwa na matatizo ya mafuriko makubwa yaliyotokea mwaka 2011.

Mbali na kutaja misaada mingi katika sekta ya miundombinu na hasa barabara ambayo imefadhiliwa na Japan katika miaka mingi iliyopita, Mheshimiwa Okada amesema kuwa Japan sasa iko tayari kuanza ujenzi wa Barabara ya Gerezani-Bendera Tatu, Dar Es Salaam, utakaogharimu Sh. bilioni 18.5, msaada kutoka Japan.

Aidha, Balozi huyo amewaomba radhi Watanzania kutokana na ucheleweshaji wa kuanza kwa ujenzi wa barabara ya juu kwa juu –flyover- katika eneo la TAZARA, Dar Es Salaam, ambao utagharimu Sh. bilioni 53 ambazo zinatolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la JICA.

Amesema kuwa ujenzi huo umechelewa kwa sababu makandarasi wa Kijapan ambao walitakiwa kujenga flyover hiyo wanakabiliwa na kazi nyingi huko nyumbani za kujenga upya miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kimbunga cha Great East Japan Earthquake and Tsunami, kilichotokea Machi 2011 na kusababisha uharibifu mkubwa mno.

Aidha, amesema kuwa wajenzi hao pia wanalazimika kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miundombinu ya kuiwezesha Japan kuandaa Michezo ya Olimpiki ambayo imepangwa kufanyika nchini humo mwaka 2020.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2014.

Picha na Taarifa Rasmi Kutoka Bunge la Katiba Mjini Dodoma:Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar

s

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar.
-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE MAALUM  

Kumekuwa na Taarifa potofu zinazosambazwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii ya kuwaMwanasheria Mkuu Zanzibar Othman Masoud Othman amekamatwa baada ya kupiga kura ya hapana Bungeni leo”. 


 
Tunapenda kuutarifu Umma wa Watanzania kuwa, taarifa hizo sio sahihi na ni porojo zenye kutaka kuleta hisia potofu kwa wananchi kuhusu kiongozi huyo.
 
Ukweli wa Jambo hili ni kuwa Mhe. Othman Masoud Othman ametekeleza haki yake ya Kidemokrasia  ya kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekeza katika Bunge Maalum leo.  Ambapo katika kura alizopiga, ameweza kuzikubali baadhi Ibara na kuzikataa ibara nyingine katika rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
 

 
Pengine hatua hiyo ya kuzikataa baadhi ya Ibara, haikuwafurahisha baadhi ya Wajumbe na hivyo kuleta majibishano ndani ya Bunge Maalum wakilalamikia uamuzi wake huo.
 

 
 
Kutokana na hofu hiyo ya baadhi ya Wajumbe kuanza kupinga uamuzi wake huo ndani ya Bunge, Ofisi ya Bunge Maalum kama ilivyokawaida kwa kila mjumbe, imeweza kumpatia Ulinzi Maalum wakati akitoka Bungeni hadi alipoondoka katika viwanja vya Bunge ili asiweze kubugudhiwa kwa namna yoyote ile kutokana na  uamuzi wake huo.
 

 
Suala hili limechukuliwa kipropaganda na kuanza kueneza uongo katika mitandao ya kijamii kuwa Mhe. Othman amekamatwa baada ya kupiga kura ya hapana.
 

 
Tunapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa Mhe. Othman hajakamatwa bali alipewa ulinzi katika Maeneo ya Bunge Maalum jambo ambalo hufanyika kwa kila mjumbe ambaye kwa namna moja ama nyingine itaonekana kuna dalili za kubugudhiwa katika Maeneo ya Bunge kutokana na uamuzi au kitendo alichofanya. Na kutokana na hali ilivyo, ulinzi wake umeimarishwa pia mahali alipo kwa hivi sasa mpaka atakapomaliza kazi yake hapa Dodoma.
 

 
Kanuni za Bunge Maalum zimempa madaraka Katibu wa Bunge Maalum kusimamia masuala yote ya Ulinzi na Usalama kwa Wajumbe na Maeneo yote ya Bunge Maalum.
 

 

 
Imetolewa na Idara ya Habari
 
Ofisi ya Bunge Maalum
 
Dodoma
 
1 Oktoba, 2014

MAONESHO YA FILAMU YALIYODHAMINIWA NA TIGO YAMALIZIKA KWA KISHINDO JIJINI ARUSHA

Mtalaam wa Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu (kulia) akikabidhi tuzo ya 'Tigo Best Short Film' kwa Mtayarishaji wa Filamu kutoka Kenya Mark Maina katika Maonesho ya Filamu ya Kiafrika Arusha (AAFF) aliyeshinda kupitia filamu yake mpya iitwayo "Consigned to Oblivion." Maonesho hayo yaliyodhaminiwa na Tigo yalifikia tamati juzi. 


2. Mratibu wa maonesho ya AAFF Nassir Mohamed akionyesha tuzo aliyoipokea kwa niaba ya Muongozaji filamu kutoka Tanzania Amil Shivji aliyeshinda tuzo ya 'Best Short Film' kwa ukanda wa Afrika Mashariki kupitia filamu yake mpya iitwayo "Samaki Mchangani." Akishuhudia kulia ni Mtalaam wa Mawasiliano wa Tigo Amani Nkurlu.

Wacheza filamu kutoka nchi za Afrika Mashariki (Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya, Tanzania na Zanzibar) wakionesha vyeti vyao ya kuhitimu mafunzo maalum ya uchezaji na uandaaji wa filamu kutoka wagwiji mbali mbali wa uandaaji wa filamu barani Afrika

 Wageni waalikwa mbali mbali na wapenzi wa filamu wakipata burudani kutoka kundi la Reggae kutoka Tanzania, Kenya na Marekani 'The Warriors from the East' wakitoa burudani.

Steve Nyerere: “Bongo movie watanikumbuka….”

MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa ana mengi ya kujivunia katika klabu hiyo ambayo anaamini yatawafanya wasanii wakumbuke kipindi cha uongozi wake.
Msanii wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Msanii wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Akipiga stori na paparazi wetu, Steve alisema kuna vitu vingi ambavyo ameifanyia Klabu ya Bongo Movie ikiwemo kurudisha heshima katika jamii kwa ujumla kuwa klabu hiyo haihusiani na vitendo vya kifuska bali ni wasanii wanaojiheshimu na kuthamini kazi zao kwa kukemea maovu.
“Naamini wasanii wa Bongo Movie watanikumbuka kwa mengi niliyowafanyia, hata kama wanatazama mabaya yangu lakini yapo na mazuri ambayo ni wazi hayapingiki, niliondoa matabaka pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ni wazi jinsi ilivyo sasa ni tofauti na nilivyoingia madarakani, nimewakutanisha na fursa mbalimbali na kusimamia nidhamu,” alisema Steve.

Steve Nyerere: “Bongo movie watanikumbuka….”

MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa ana mengi ya kujivunia katika klabu hiyo ambayo anaamini yatawafanya wasanii wakumbuke kipindi cha uongozi wake.
Msanii wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Msanii wa filamu Bongo aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’
Akipiga stori na paparazi wetu, Steve alisema kuna vitu vingi ambavyo ameifanyia Klabu ya Bongo Movie ikiwemo kurudisha heshima katika jamii kwa ujumla kuwa klabu hiyo haihusiani na vitendo vya kifuska bali ni wasanii wanaojiheshimu na kuthamini kazi zao kwa kukemea maovu.
“Naamini wasanii wa Bongo Movie watanikumbuka kwa mengi niliyowafanyia, hata kama wanatazama mabaya yangu lakini yapo na mazuri ambayo ni wazi hayapingiki, niliondoa matabaka pamoja na kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ni wazi jinsi ilivyo sasa ni tofauti na nilivyoingia madarakani, nimewakutanisha na fursa mbalimbali na kusimamia nidhamu,” alisema Steve.

Mwanafunzi afariki baada ya kuangukiwa na kifusi….


MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA KATIKA SHULE YA MSINGI SANZYA WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VALIUD SIAME KIMUNDE (13) MKAZI WA KIJIJI CHA KAONGA ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA KIFUSI CHA MCHANGA.
kifusi
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.09.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAONGA, KATA YA CHILULUMO, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, WAKATI TUKIO HILO LIKITOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA WANAFUNZI WENZAKE WAKICHIMBA NA KUBEBA MCHANGA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA KULALA WAALIMU SHULENI HAPO.
MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI KWA KUTOA UANGALIZI WAKUTOSHA IKIWA NI PAMOJA NA KUWASIMAMIA WATOTO KATIKA SHUGHULI WANAZOWATUMA KUFANYA ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

Wednesday, October 1, 2014

Facebook hatimaye yapata mpinzani


Ello

Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaazishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.
Mtandao huu kwa mjibu wa muanzilishi umeanzishwa August mwaka huu ukiwa ambapo hauna gharama yoyote kwa mtumiaji iwe matangazo ama kulipia data.
Hata hivyo baadhi ya watumiaji wameubatiza kwa jina la Anti-Facebook mtandao huo, wakimaanisha kwamba ndiye mpinzani mkubwa wa Facebook.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya kimitandao wamekosoa mfumo wa Ello kutotoza gharama yoyote wakidai kuwa katika siku za usoni huenda mtandao wa Ello utalazimika kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa watumiaji wake.
Paul Budnitz mtengenezaji wa baiskel za kampuni ya Vermont ameiambia BBC kuwa wapo imara katika ushindani wa kimitandao na kujigamba kuwa ana wataalamu wa kutosha kukabiliana na makampuni pinzania.
Hata hivyo kuhusiana na baadhi ya watu kuuiita kwa jinala bandia la anti-Facebook mtandao huo yeye amesema wanajiendesha kama mtandao wenye mtazamo wake binafsi na si kutegemea mtazamo wa mtandao wa Facebook.

Mke wa rais wa Zimbabwe kushtakiwaGrace Mugabe kulia
Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa.
Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.
Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.
Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia

BBC SWAHILI

MAJAJI WAENDESHA MAHAKAMA YA WAZI KUSIKILIZA NA KUPOKEA MALALAMIKO YA WAKULIMA WALIONYANG'ANYWA ARDHI,WAFUGAJI NA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI LEO

 
Jaji Mh. Richard Mziray Akitoa Hukumu katika Mahakama ya wazi  katika Kesi zote Mbili ya Kiteto na Kilosa ,ambapo katika Kesi ya Wilaya ya Kiteto alitoa Maamuzi kwamba kulikuwa na umuhimu wa utekelezeji wa Amri ya Mahakama na kuheshimu Amri za Mahakama kuwa Mahakama ilisha tamka kuwa ile ni Hifadhi hivyo inatakiwa kulindwa na kuheshimiwa na ameongeza kuwa kama kungekuwa na kuzingatiwa kwa Sera za Ardhi basi kusingekuwa na Migogoro yote hiyo ametolea mfano pia maeneo ambayo yanatakiwa kulindwa ni pamoja na Bahari na Hifadhi.Katika kesi ya Kiteto alimalizia kuwa Maamuzi ya Mahakama yangeheshimiwa basi kungekuwa hakuna hii Migogoro yote.
Katika Kesi ya Kilosa Mh. Jaji Richard alisema kwamba Mgogoro uliopo ni juu ya Maji katika Mto wa Mkondoa na Muyombo ambao unagombaniwa wa wafugaji pamoja na wakulima na kwamba katika mgogolo huu Serikali inapendelea zaidi Wakulima na kuwaacha wafugaji alisema kwamba ikiwa wafugaji wangekuwa wanasababisha uharibifu wa Mazingira basi wasinge Ruhusiwa kutumia mito hiyo na hakuna sehemu inaonesha wafugaji wanaharibu Mazingira. Hivyo wafugaji wanahaki ya kutumia mto huo.
Mwisho katika kesi zote Mbili Mh. Jaji  Richard Mziray alitoa Tamko lifuatalo kuwa Wafugaji wanahaki sawa ya kutumia mito hiyo, pia wafugaji wanahaki ya kushiriki katika maamuzi ya wakulima , Wanao lazimisha mkondo wa mito hiyo uende sehemu ambayo sio yake hawana mamlaka ya kufanya hivyo Mwisho ameshauri kwamba ili migogoro hii isiweze kuendelea kuna umuhimu wa upendo kwanza Baina ya pande zote Mbili wakilima na Wafugaji, wakifanya hivyo kutakuwa hakuna migogoro kulipo kungoja Amri za Mahakama.
 Majaji wakiwa wanasikiliza Kesi kwa Makini juu ya migogoro ya Ardhi na wafugaji, Wawekezaji wanachukua maeneo ya wanavijiji, Unyang'anyi wa ardhi na Mazingira kwa ujumla  Kutoka kushoto ni Mh. Jaji msaidizi Jonas, wa katikati ni Mh. Jaji Richard Mziray, na Mh.Jaji Msaidizi Emma Lukumai
 Muwezeshaji wa Mkutano huu Jenerali Ulimwengu akiendelea kutoa Mwongozo
Mlalamikaji wa Kesi ya matukio makubwa katika hifadhi za Murtangos na Sulendo Wilayani Kiteto Bwana Lembulu Ole Kosyamlos  kushoto akitoma malalamiko juu ya hifadhi ya E-Murtangos iliyoundwa na vijiji saba ambavyo ni Kimana,Ndirkishi, Emarti,Nhati, Engusero,O-sidan na Loltepesi ambapo walianza mchakato huo mwaka 1996 na kurasimishwa rasmi Mwaka 2002 na hifadhi hiyo inaukubwa wa Hekta za Mraba 133,33.15, alieleza changamoto za wafugaji na wakulima ambapo watu wengi walipoteza maisha,Wavamizi kuingia bila utaratibu na kuharibu mazingira, na wimbi la uvamizi kuendelea siku hadi siku mpaka kufikia mwaka 2013. Pia katika Mashitaka hayo ameiomba mahakama ya wazi iwasaidie kutatua tatizo lao na Serikali iangalie upya eneo hilo Kisheria na zisiingizwe Sheria katika Jambo Hilo.
Mh. Diwani lairumbe Mollel ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akitoa Malalamiko yao Mbele ya Mahakama ya wazi juu ya Hifadhi ya Msitu wa Vijiji Lusendo ambapo alieleza kuwa hifadhi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1994/1995 ambapo vijiji 9 viliungana na kutengeneza hifadhi hiyo aliongeza baada ya kuanzisha hifadhi hiyo walipata mafanikio ikiwa ni pamoja na kujipatia fedha kupitia uvunaji wa miti , mkaa endelevu na asali , pia walifanikiwa kupata Gari moja aina ya Land Cruzer Pick up na pikipiki . Alimalizia kwa kuleta malalamiko yake katika Mahakama ya wazi kuwa kuna uvamizi uliokithiri kwa maeneo ya Misitu Hususani Maeneo yote yanayozunguka mipaka ya Wilaya za Kilindi na Kiteto na Kuiomba Serikari wapate kurejeshewa maeneo yao.
Bwana Henry Parmeo akitoa mashitaka yake Mbele ya Mahakama ya wazi  juu ya mgogolo uliopo Kilosa kati ya wafugaji na wakulima hasa katika eneo la maji, na muwekezaji ambaye yeye amebadilisha Mkondo wa Maji kutoka katika eneo lake husika na kwenda katika Mashamba, Katika kesi hiyo amedai kwamba wakulima wamekuwa wakiwalaumu wafugaji hao kuwa ndio wenye makosa kwa kuwa wanaingilia wakulima kuwa Mifugo yao inakula mazao na kusahau kwamba Wakulima hao wamebadilisha mkondo huo kwenda mashambani, na aliongeza kuwa mgogoro huu huwa unajitokeza hasa wakati wa kiangazi miezi ya Nane,Tisa, Kumi, Kumi na moja na Kumi na Mbili katika mto Mkondoa na Myumbo. ameiomba Mahakama ya wazi pamoja na Serikali kumaliza Mgogoro huu.
Mama Shujaa wa  Chakula kutoka Mkoa wa Morogoro akielezea kwa kina zaidi juu ya Mgogoro wa wakulima na wafugaji hasa katika mito miwili ambapo wote wanagombania kupata maji hasa wakati wa kiangazi na amewapongeza Oxfam kwa Juhudi zao za kusaidia kutatua matatizo ya Mgogoro huo
Bi Vera F. Mugittu Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina zaidi Juu ya Kesi Mbili zilizotajwa Kesi ya Kilosa na Kiteto na kusema kuwa Migogoro yote ni Juu ya Lasilimali na kwamba Serikali pamoja na Mahakama wanatakiwa kujua Matatizo haya na kujua Jinsi gani wanaweza kuyatatua na kuwajengea uwezo watu wapate kujitambua ili kuepukana na migogoro hiyo, Alimalizia kwa kusema kuwa ucheleweshaji wa kusikiliza kesi ndio unao ongezea Migogoro.
Bwana Muro Mjumbe wa Bodi ya Forum CC akitoa maelezo ya kina juu ya kesi mbili za Kilosa na Kiteto
Baadhi ya Wachangiaji wakichangia Michango na mawazo mbalimbali wakati wa Mahakama ya Wazi iliyo andaliwa na Oxfam pamoja na Forum CC
Mh. Emma akitoa ufafanuzi juu ya Vifungu mbalimbali vya Sheria wakati wa Hukumu hizo katika mahakama ya wazi leo
Mh.  Jonas akitoa ufafanuzi zaidi wa maamuzi katika kesi hiyo ya Mahakama ya wazi
 Michoro ambayo inaonesha matukio mbalimbali ya Mkutano huo
 Burudani ikiendelea wakati wa mapumziko mafupi
Baadhi ya watu wakiwa wanasikiliza kesi kwa makini katika Mahakama hiyo ya wazi ambayo iliandaliwa na Oxfam na Forum CC