Askari waliokuwa katika msafara huo wakisaidia kuongoza magari eneo hilo

Basi la Abood likiwa limepinduka jioni ya leo huku majeruhi wakiokolewa
Ajali mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Visiga mkoani Pwani baada ya basi la kampuni ya Abood lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda morogoro Kuacha njia na kupinduka .

Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Pwani Bw C. Mtoye anaripoti kuwa basi hilo limepinduka muda mfupi wakati likipisha msafara wa unaosadikika kuwa wa mmoja kati ya viongozi wa kitaifa ambao ulikuwa ukitokea barabara ya Morogoro - Dar es Salaam.

Katika ajali hiyo jumla ya abiria zaidi ya 30 wamejeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakinusurika katika ajali hiyo .
   CHANZO::FRANCISS GODWIN BLOG

Post a Comment

 
Top