Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ameunda kamati ya kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutaka apewe matokeo ndani ya saa 24.

Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari  mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.

 “Matukio kama haya hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa, lakini kama Rais yupo na nchi haijapinduliwa  basi kuingia ndani ya chombo cha habari na silaha, huku ni sawa na kunajisi uhuru wa habari,” alisema Nape

Post a Comment

 
Top