Wakazi wa Kinondoni  Mahakamani wamelalakia maji yaliyozingira nyumba zao kutokana na baadhi ya wakazi hao kujenga katika mkondo wa maji.

Akizungumza leo mkazi wa eneo hilo Bi. Khadija Hamis amesema kutokana na mvua za  masika zinazoendelea kunyesha wanapata adha kubwa ya maji hayo yanayotuama kwenye eneo hilo.

Amesema kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamezingirwa na maji kwa wiki mbili sasa na hakuna chochote kinachofanyika.

Aidha amesema kutokana na hali hii kuendelea ,wanaiomba serikali kutatua tatizo hili mara baada ya kuisha masika.

Mvua zinazoendelea  kunyesha  maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam iliyoanza kunyesha wiki iliyopita, zimesababisha maafa, uharibifu wa miundombinu ya baarabara pamoja na baadhi nyumba katika eneo la Kinondoni Mahakamani kuzungukwa na maji ya mvua  jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top