Mrembo Karrueche Tran amekana kuhusika katika ugomvi unaoendelea kati ya ex wake Chris Brown na kundi la Migos kutokana na tetesi za kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Quavo.

Mrembo huyo alipoulizwa kuhusu ugomvi wa wasanii hao uliotokea baada ya katika BET after Party, amedai yeye hausiki kwa chochote kwenye hilo. Karrueche aliuambia mtandao wa TMZ Jumatano hii wakati alipokuwa uwanja wa ndege mjini Los Angeles akitimka.

Siku ya Jumanne kupitia mtandao huo, ulisambaza video zikiwaonyesha watu wakirushiana makonde ambao wanadaiwa kuwa ni moja ya wapambe wa Chris waliowaanzishia vurugu wasanii wa kundi hilo.


SOURCE; BONGO5

Post a Comment

 
Top