Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akitoa elimu ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 400 wa kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani Mkoani Iringa
 Baadhi ya vijana walishiriki katika mafunzo ya kupewa elimu ya ujasiliamali katika kanisa la parokia ya Ismani


Na Sebastian emmanuel jr, kwa msaada wa Fred Mgunda, Iringa

Zaidi ya vijana mia nne (400) wa kikatoriki kutoka katika parokia kumi zinaizunguka Manispaa ya Iringa wamepata elimu ya ujasiliamali kutoka kwa mbunge wa viti maalum Mkoani kupitia chama cha mapinduzi (CCM).

Mafunzo hayo yametolewa katika Kanisa la kikatoriki parokia ya Ismani linaloongozwa paroko Leonard Maliva.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo mbunge wa viti maalumu Ritta Kabati alisema kuwa ujasiliamalia ni kitendo mtu yeyeto yule kutumia fursa ipasavyo pamoja na kuwa na nidhamu ya kuzitumia vizuri fursa unazipata.

"Leo hii tupo hapa Ismani kuna changamoto nyingi sana ambazo hazijapatiwa ufumbuzi hivyo inatakiwa kuzibarisha changamoto hizo kuwa mtaji wako kwa kubuni kitu ambacho kitakuletea faida hapo ndio utaanza kuitwa mjasiliamali"alisema Kabati

Kabati aliwataka vijana kuacha kutumiwa na wanasiasa kwa sababu wanasiasa wengi wapo kwa ajili ya maslai yao na sio kumtetea kijana hivyo vijana wanapaswa kutumia akili sana anapofanya kazi na wanasiasa.

"Ukitawa utafuna bigijii mwanzoni huwa inakuwa na utamu ila mwishoni utamu unaisha ndio hata sisi wanasiasa ndio tunavyowatumia vijana kwa maslai yetu" alisema Kabati

Aidha Kabati aliwaambia washiriki wa elimu hiyo ya ujasiliamali kukubali hasara wanapoanza ujasiliamali wao kwa kuwa vitu vingi vianakuwa vigeni kwao hivyo lazima uwe mvumilivu katika hali ngumu na hali ya faida.

Kabati aliwataka vijana kuacha kutumia vibaya pesa wanazipata kwenye biashara kwa kuwa ukifanya hiyo utakuwa unapunguza mtaji na hatimaye wanajikuta wamefilisika .

"Leo umepata faida kubwa lakini faida yote unaipeleka kula starehe ambayo haina faida kwa na kujikuta kila siku unataka kushindana na matajili wenye uwezo wako hivyo pesa inataka nidhamu ya hali juu kwa sababu hata nyie ni mashaidi huko majumabini kwenu kuna watu walikuwa na matajili lakini wamefilisika kutokana kutumia pesa bila nidhamu "alisema Kabati

Salvatory Komba,Lameck Lugala,Bariki Matonya,Francisco Mhehe na Odeth Kikoti ni baadhi ya washiriki waliohudhuria elimu hiyo ya mjasiliamali na kuwapongeza viongozi kuwa kuwakutanisha vijana na kuwapa elimu yenye faida kubwa kwenye maisha.

"Leo hii tumenufaika na elimu hii kutoka kwa mbunge na viongozi wengine ambao wametufundisha vitu vingi tuwaombe vijana wenzetu kufanya kazi kwa kujituma na kuitumia katika kujiletea maendeleo binafsi na ya nchi" walisema baadhi ya washiriki

Washiriki hao wasilisema kuwa ukifuatilia kwa makini mafunzo ya ujasiliamali yanafaida kubwa kwenye maisha yetu.

Kwa upande wake paroko Leonard Maliva wa parokia ya Ismani alimushukuru mbunge huyo kwa elimu aliyoitoa na kuwaomba vijana kuieshimu na kuitumia vizuri kwa ajili ya kuongeza maarifa vichwani mwao.

Maliva alisema kuwa kila mwaka wamekuwa wakitoa elimu ya maisha kwa zaidi ya vijana elfu moja kwa lengo la kuisaidia serikali kupata vijana wenye elimu ya dunia pamoja na elimu ya dini hivyo ukiwa na vijana wanaojituma kufanya kazi huku wakiwa na nidhamu basi nchi itapata maendeleo kwa kazi.

Post a Comment

 
Top