SeeBait

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa.
Taarifa iliyotolewa  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John Eudes Ruhangisa kuanzia  06 Julai, 2017.
Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya  Tanzania kanda ya Shinyanga.
Gerson MsigwaMkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULUDar es Salaam

Post a Comment

 
Top